Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema ambaye alishtakiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya viongozi wa serikali, leo November 8 amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Arusha na kusomewa shtaka linalomkabili baada ya kukaa mahabusu kwa siku saba.
Hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi anayesikiliza kesi hiyo Desdery Kamugisha amesema hawezi kutolea maamuzi kwenye mahakama hiyo kwa kuwa anahitaji muda wakusoma na kupitia vifungu vya sheria na hoja zilizotolewa na November 11 atatoa maamuzi.
Kutokana na hatua hiyo Godbless Lema amerudishwa rumande hadi November 11 mwaka huu. Wakili wa Chadema John Malya amesema kutokana na hoja zote zilizowasilishwa kwa pande zote mbili zimeonekana zina uzito hivyo wanasubiri uamuzi wa mahakama.
Mbunge Lema amefikishwa mahakamani leo na kusomewa shtaka la uchochezi dhidi ya viongozi wa serikali baada ya kukaa mahabusu kwa siku saba pic.twitter.com/FVWD9Kq3HX
— millardayo (@millardayo) November 8, 2016
Baada ya Lema kufikishwa mahakamani leo, wakili wa CHADEMA, Malya amesema wanasubiri uamuzi wa mahakama ambapo uamuzi utatolewa Nov 11 2016 pic.twitter.com/RflJynVoKY
— millardayo (@millardayo) November 8, 2016
ULIKOSA HII YA POLISI KUSEMA HATI YA KUMKAMATA LISSU HAIJATUFIKIA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI