Baada ya headlines za usajili kuzidi kushika kasi Bongo, Singida United wameendeleza kushusha vifaa ili kuboresha safu ya ulinzi na ushambuliaji ya timu yao, Singida United leo imtambulisha rasmi Danny Usengimana kutoka Polisi FC ya Rwanda na Michel Rusheshangonga kutokea APR FC.
Danny Usengimana anayecheza nafasi ya ushambuliaji ndio mchezaji anayeshikilia rekodi ya ufungaji bora kwa mara mbili mfululizo katika Ligi Kuu Rwanda, wakati Michel anayecheza beki wa kulia anacheza timu ya taifa ya Rwanda kama ilivyo kwa Usengimana.
Michel hadi anaondoka APR FC na kuja kujiunga na Singida United alikuwa ndio nahodha wa APR FC, wote kwa pamoja Danny na Michel baada ya utambulisho huo wameunganisha ndege kuelekea Mwanza kuungana na wachezaji wenzao katika maandalizi ya Ligi Kuu 2017/18.
EXCLUSIVE: Staa wa Bundesliga mwenye asili ya Tanzania kwanini anachezea Denmark na sio Tanzania