Baadhi ya michezo ya awali ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imechezwa leo, moja kati ya mchezo wa marudiano uliyochezwa leo ni mchezo kati ya Yanga dhidi ya St Louis ya Ushelisheli, mchezo ambao umechezwa katika uwanja wa Linite katika mji wa Victoria nchini Ushelisheli
Yanga akiwa ugenini alikuwa anaenda kutafuta sare yoyote ili aweze kufuzu, hivyo tahadhari ilikuwa kubwa zaidi kwao kutokana na mchezo wao wa kwanza uliyochezwa Dar es Salaam, walipata ushindi wa goli 1-0, hivyo mchezo wa leo uliwahitaji umakini mkubwa ili kufuzu na kusubiria kujua mshindi kati ya AL Mereikh ya Sudan na Township Town ya Botswana watacheza na nani.
Pamoja na kuwa Yanga walikuwa ugenini na wenyeji wao St Louis wakiwa na sapoti ya mashabiki, wamejikuta wakilazimishwa sare ya kufungana 1-1 baada ya kujisahau, Yanga walipata goli la kuongoza kupitia Ibrahim Ajibu dakika ya 45 lakini dakika za nyongeza kabla ya game kuisha St Louis wakasazisha goli hilo ila Yanga wamefuzu kwa ushindi wa jumla ya magoli 2-1.
Naambiwa haya ndio magari ya Mbwana Samatta anayotumia Ubelgiji