Baada ya kusimama kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia kumalizika kwa hatua ya Makundi, usiku wa February 13 2018 michuano hiyo iliendelea tena kwa michezo miwili ya hatua ya 16 kuchezwa, Man City walikuwa ugenini dhidi ya Basel na Totteham Hotspurs walikuwa wageni wa Juventus.
Mchezo wa Tottenham Hotspurs dhidi ya Juventus ndio mchezo uliyokuwa unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi kuliko mchezo wa Basel na Man City, hisia ambazo zimekuwa kweli na hadi dakika ya 90 zinamalizika game hiyo ilikuwa 2-2, hivyo kazi imebaki katika mchezo wa marudiano katika uwanja wa Wembley.
Juventus ambao walikuwa nyumbani walionekana kuanza vizuri baada ya Gonzalo Higuan kuifungia magoli dakika ya 2 na dakika ya 9 ya mchezo kitu ambacho kiliwachanganya mwanzoni Tottenham lakini Higuan pia alikosa tena penati dakika ya 45.
Upepo ulibadilika dakika ya 35 baada ya Harry Kane kuifungia goli la kwanza Tottenham dakika ya 35 kwa kutumia vyema pasi safi ya Dele Alli, goli hilo liliwarudisha mchezoni na dakika ya 72 Christian Eriksen aliisawazishia Tottenham kwa mkwaju wa faulo, hata hivyo goli la Harry Kane limemfanya kuifikia rekodi ya Steven Gerrard aliyoiweka msimu 2008/9.
Kane sasa baada ya kufunga goli hilo ameifikia rekodi ya Steven Gerrard ya kuwa mchezaji wa England aliyefanikiwa kufunga magoli mengi katika msimu mmoja wa UEFA Champions League kwa kufunga jumla ya magoli 7 sawa na Steven Gerrard aliyeiweka rekodi hiyo msimu 2008/9 akiwa na Liverpool, hadi game inaisha Spurs alikuwa anatawala mpira kwa asilimia 67 kwa 33.
VIDEO:Magoli ya Simba walivyorudi kimataifa leo vs Gendermarie Full Time 4-0