Kwa muda mrefu kumekuwa na headlines zilizodaiwa kuwa ni mvutano kuhusiana na staa wa soka wa Kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona ya Hispania, Neymar kudaiwa kushinikiza kuihama Klabu hiyo na kujiunga na Paris Saint Germain ya Ufaransa.
Leo August 2, 2017 FC Barcelona wamethibitisha kumpa ruhusa Neymar kutofanya mazoezi na timu ili kuelekea kukamilisha usajili wake wa kujiunga na PSG ingawa taarifa ya Barcelona haijaweka wazi sababu za moja kwa moja za ruhusa hiyo.
Baada ya ruhusa hiyo vyombo vingi vya habari Ulaya vinaripoti kuwa Neymar anaelekea kuanza safari yake ya maisha mapya PSG ambao wameripotiwa kutenga pound Milioni 199 kwa ajili ya kuvunja mkataba wa staa huyo wa zamani wa Santos kiasi kilichopo katika mkataba wake.
Kama uhamisho huo ukikamilika Neymar ndio atakuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kuuzwa katika historia ya soka. Kwa kiasi cha pound milioni 199 anachouzwa Neymar ni zaidi ya Tsh Bilioni 580 kiasi ambacho hajawahi kuuzwa wala kununuliwa mchezaji yeyote katika historia.
VIDEO: Gor Mahia vs Everton: Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017)