Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara imemhukumu kifungo cha miaka 13 Jela, mshitakiwa Shaibu Ally Mtepa (64) kwa kosa la kujaribu kuua na kumjeruhi kwa kumkata viganja vya mikono aliyekuwa Mke wake Fadina Mussa, ambao wote ni wakazi wa kijiji cha Malopokelo Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara.
Kesi hiyo namba 11ya mwaka 2023, imetolewa hukumu yake na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mwenye Mamlaka ya Ziada, Frederick Lukuna.
Mshitakiwa huyo anatajwa kutenda kosa hilo December 03, 2021 wilayani Tandahimba baada ya kumpa talaka Mkewe huyo na Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara kuwaamuru wanandoa hao kugawana mali walizochuma ambao wakiwa kwenye hatua hiyo ya mgawanyo ndipo Mtuhumiwa alipofanya tukio hilo la kumkata mapanga Fadina.