Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imesema haina mamlaka ya kutoa amri ya kuzuia Bunge kutowaapisha Wabunge wapya 8 wa Chama cha Wananchi, CUF walioteuliwa kuziba nafasi za Wabunge wa Viti Maalumu waliofutwa Uanachama.
Hatua hiyo inatokana uamuzi wa Jaji Lugano Mwandambo ambaye ametupilia mbali maombi ya Wabunge 8 na Madiwani ambao walikuwa wanapinga kuapishwa kwa Wabunge wapya kuziba nafasi zao.
Jaji Mwandambo amesema Mahakama hiyo na Bunge vinafanya kazi kwa mujibu wa Katiba na kusema anatambua katika maombi ya Wabunge 8 na Madiwani waliofutwa Uanachama hawakuiomba Mahakama kuinyang’anya Bunge Mamlaka ya kuwaapisha Wabunge wapya.
“Hivyo kuna mashiko katika pingamizi la serikali na ninakubaliana nao kwamba haina mamlaka ya kulizuia Bunge kuwaapisha Wabunge hao.”
Hata hivyo, Jaji Mwandambo amesema uamuzi huo haumaanishi maombi ya mapingamizi mengine ya Wabunge na Madiwani hao hayatosikilizwa, ambapo yataanza kusikilizwa August 31, 2017.
Wabunge hao walikuwa wakipinga kutoapishwa kwa Wabunge 8 walioteuliwa na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC.
ULIPITWA? MAHAKAMA KUU KUHUSU WALE WABUNGE 8 WA CUF!!!
WAFUASI WA CUF WALIODHIBITIWA MAHAKAMANI!!!