Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu apelekwe gerezani kwa siku saba wakati akisubiri maamuzi ya dhamana yake.Wema aliingia matatani baada ya kutofika mahakamani hapo mara mbili ambapo mahakama hiyo ilitoa hati ya kumkamata kwa kuruka dhamana.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.Kesi imeahirishwa hadi Juni 24, 2019.”Kesi hii itakuja Juni 24, mwaka huu hivyo inabidi mshitakiwa ukae ndani hadi tarehe hiyo,” alisema Maira Kasonde.
Akijitetea kwanini asifutiwe dhamana, Wema amedai ni kweli hakufika mahakamani Mei 11 na Juni 14, mwaka huu. Wema alidai mara ya kwanza alisafiri kikazi nje ya mkoa ambapo alikwenda mkoani Morogoro na kwamba alimpa taarifa wakili wake.
Pia alidai mara ya pili, alifika mahakamani lakini alishindwa kuingia kwenye chumba cha mahakama kusikiliza kesi yake kwa sababu aliumwa ghafla tumbo la hedhi. Alidai anapofika tarehe ya hedhi mara nyingi tumbo humuuma hivyo alienda hospitali kwa ajili ya kuchomwa
sindano ya diclopa.
Hata hivyo, aliomba mahakama imsamehe kwa kutokuhudhuria mahakamani.Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai mshitakiwa hana rekodi yakutohudhuria mahakamani hivyo mahakama impe onyo. Wema anakabiliwa na mashitaka la kuchapisha video ya ngono katika mtandao wa kijamii.
Wema anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhui.
AUDIO: HALIMA MDEE ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI “NIMEIMARIKA KWA KASI YA AJABU”