Staa wa timu ya taifa ya Chile anayekipiga katika club ya Man United ya England Alex Sanchez ikiwa club yake inaelekea kucheza mchezo wa round ya tano wa Kombe la FA dhidi ya Chelsea, kocha wa muda wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjaer amemfananisha mchezaji huyo na chupa ya tomato (Ketchup).
Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda Alex Sanchez anatarajiwa kuwa sehemu ya wachezaji wa Man United watakaopata nafasi ya kucheza mchezo huo dhidi ya Chelsea, kauli ya Solskjaer inalenga kumfariji mchezaji huyo na kumfanya arudi mchezoni na makali kuelekea mchezo dhidi ya Chelsea.
Sanchez amefunga magoli mawili katika michezo 19 na mingi kati ya hiyo amekuwa akitokea bechi, hivyo kwa mchezaji anayelipwa mshahara wa pound 350000 kwa wiki ni takwimu mbaya hususani akiwa ana miezi 13 ndani ya Man United toka ajiunge nayo January 2018 akitokea Arsenal, hivyo game ya Jumatatu dhidi ya Chelsea atapewa nafasi ya kuanza kwa kukosekana kwa Athony Martial na Jesse Lingard.
“Sanchez ni kama chupa ya Ketchup (Tomato Sauce) sasa ipo tayari kutolewa” kauli ambayo ameisema Ole Gunnar Solskjaer inatafsrika kuwa Sanchez ana kipaji kikubwa kimejaa na sasa baada ya kurudi uwanjani yupo tayari kukionesha katika game dhidi ya Chelsea.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba