Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi timu ya taifa ya Afrika Kusini July 6 2019 ilicheza mchezo wake wa 16 bora dhidi ya wenyeji Misri, game hiyo ilimalizika kwa Afrika Kusini kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Lotch dakika ya 85 ya mchezo huo, baada ya game kocha wa Afrika Kusini muingereza Stuart Baxter aliongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa mbinu yao iliyowaidia ni kuhakikisha wanashirikiana kuzuia mipira isifike kwa MO Salah na Trezeguet.
“Tulijaribu kuhakikisha tunazuia mipira kwenda kwa MO Salah na Trezeguet na nafikiri tulifanya vizuri, game dhidi ya Nigeria itakuwa ni changamoto kubwa tutajitahidi kadri ya uwezo wetu asante”>>> Stuart Baxter
Baada ya ushindi huo timu ya taifa ya Afrika Kusini sasa inajiandaa kucheza robo fainali ya AFCON 2019, dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria ambayo imeingia hatua ya robo fainali kwa kuiondoa Cameroon ambao ni mabingwa watetezi kwa kuwafunga kwa magoli 3-2.
VIDEO: Kinachomfanya Bongo Zozo asite kuomba uraia wa TZ, Maisha yake?