Benki ya BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara leo imeendelea kudhihirisha ubunifu wake katika huduma zinazowanufaisha wateja wake baada ya kutangaza kuzindua akaunti mpya ya IZZE ambayo ni rahisi kufungua na haina makato yeyote ya mwezi.
Kwa kupitia akaunti ya IZZE ya BancABC, mteja anahitaji kuwa na kitambulisho cha taifa tu kilichotolewa na NIDA ili kufungua akaunti hiyo na atapata riba hata akiwa na kianzio cha shilingi Elfu Kumi (Tshs10,000/-)
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua akaunti hiyo, Mkurugenzi wa Biashara na Wateja wadogo na wakati wa benki BancABC Joyce Malai ‘Leo kwenye soko la biashara watu wengi wanaangalia sehemu watakayo nufaika kuwekeza fedha zao na yenye uhakika wa kupata faida/manufaa kadhaa. Uhakika wa kupata faida au manufaa ni moja ya malengo muhimu kwa kila mtanzania. Vile vile, kufungua akaunti ya benki kwa siku hizi imekuwa ikichukuliwa kama hatua ngumu yenye kuhitaji muda na zaidi inaonekana kama inalenga watu wenye kipato kikubwa”
Malai aliongeza kuwa akaunti ya IZZE ni Rahisi kufungua kama ilivyo jina lake, mteja anahitajika kuwa na kitambulisho cha taifa TU na haina kiasi chochote cha kuanzia, haina makato ya mwezi na muhimu zaidi ni kwamba mteja anapata riba kila mwezi ikiwa ana salio kuanzia shilingi elfu kumi (Tshs. 10, 000/-) au zaidi kwenye akaunti yake.
Akaunti hii imeunganisha kwenye mtandao wetu wa BancABC Mobi kupitia USSD (*150*34#) na APP kwa hivyo mteja haitaji kila mara kutembelea matawi yetu kwa ajili ya kuweka au kutoa hela. Vile vile mteja anaweza kutumia akaunti yake kupitia machine za ATM zenye nembo ya Visa, mawakala wa BancABC pamoja na “internet banking”
Mteja wa IZZE akaunti atapata huduma hizi zote za kibenki kwa masaa 24 siku saba za wiki
VIDEO: Moja kati ya magoli ya marehemu Jeba, hili liliwaumiza wana-Simba 2016