Club ya Dar es Salaam Young Africans leo ilikuwa jijini Arusha kucheza game yao ya Ligi Kuu dhidi ya African Lyon walioamua kuhama uwanja na kwenda Sheikh Amri Abeid kuutumia kama uwanja wao wa nyumbani, hiyo ni kutokana na kuamua kuondoka jumla Dar es Salaam kwa kukosa mashabiki viwanjani.
Yanga leo iliingia uwanjani kucheza game hiyo pasipo uwepo wa kocha wao mkuu Mwinyi Zahera aliyeondoka mapema wiki hii kuelekea Ufaransa kwa kile anachokiita amehitajika kwenda kusaini nyaraka za biashara zake nchini humo, Yanga bila ya uwepo wa Zahera imeifunga African Lyon kwa goli 1-0.
Goli pekee la Yanga limefungwa na Abdallah Shaibu Ninja dakika ya 64, hivyo Yanga wanaendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote hadi sasa, wamefikisha jumla ya point 47 wanaendelea kuongoza Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 nafasi ya pili bado yupo Azam FC mwenye jumla ya point 40 Simba nafasi ya tatu kwa kuwa na point 30 akizidiwa michezo minne na Yanga, Azam mitatu.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe