Baada ya shirikisho la soka Afrika CAF kutangaza mabadiliko ya waamuzi wa mchezo wa marudiano wa CAF Champions League kati ya TP Mazembe dhidi ya Simba SC uliyopangwa kuchezwa April 13 mjini Lubumbashi, uongozi wa Simba SC kupitia kwa mtendaji wao mkuu Creacentius Magori ameandika barua CAF.
Simba SC kupitia mtendaji wao mkuu wa club limeandika barua ya kutangaza hofu yake baada ya mabadiliko ya ghafla ya waamuzi wa mchezo huo, kubwa pasipo kutajwa sababu za msingi zaidi ya kueleza kuwa za kiufundi, Simba imeeleza kuwa hofu yao inakuja kutokana na waamuzi wa mchezo huo wengi wao wanatoka Zambia ambapo ni karibu sana na Lubumbashi ni mwendo wa gari.
Hivyo kutotajwa kwa sababu za mabadiliko hayo kumeanza hofu kubwa inawezekana ikawa hujuma dhidi yao, Pamoja na kuwa Simba SC wamepangwa kuchezeshwa na refa Janny Sikazwe anayetokea Zambia aliyechezesha pia Kombe la Dunia 2018.
Simba imehofia kuwa ni rahisi kwa TP Mazembe kupanga njama na waamuzi kutokana na kuwa nao karibu, kutoka Lusaka Zambia hadi Lubumbashi utakapochezwa mchezo huo ni umbali wa Kilometa 545, wakati umbali wa kutoka Dar es Salaam Tanzania kwenda Lusaka Zambia ni Kilometa 1949 hivyo TP Mazembe wapo jirani zaidi ya waamuzi kuliko Simba SC.
“Nina uhakika tunaweza kushinda Lubumbashi na kufuzu”- Kocha Simba SC