Leo club ya Man United imemtangaza rasmi aliyekuwa kocha wao wa muda Ole Gunnar Solskjaer kuwa kocha wao mpya wa kudumu kwa mkataba wa miaka mitatu, pamoja na kuwa baadhi ya watu na mashabiki wameipokea taarifa hiyo kwa furaha kutokana na Ole Gunnar Solskjaer kuanza vizuri lakini wapo watu ambao wanahisiwa kuwa hawajapenda hilo kwa sababu mbalimbali.
Baadhi ya wachezaji wa Man United hii haiwezi kuwa habari njema kwao na inaweza ikawa ndio mlango wao wa kuondokea, hii ndio list ya watu ambao wanahisiwa kuwa kuna uwezekano mkubwa hawajafurahishwa na Ole Gunnar Solskjaer kupewa mkataba wa kudumu Man United.
1- Antonio Valencia
Nahodha huyo inawezekana akawa ni mmoja kati ya watu ambao hawajafurahishwa, kwani hana nafasi kubwa sana ya kucheza kuelekea mwisho wa msimu, hivyo hiyo inaweza ikawa ni dalili ya kuondoka ndani ya club hiyo aliyodumu nayo kwa miaka 10.
2- Alex Sanchez
Pamoja na kuwa aliamini anaweza akarudi vizuri uwanjani lakini inaelezwa Solskjaer hafikirii hivyo, toka club hiyo ianze kuonesha nia ya kuwataka wachezaji Jadon Sancho na Callum Hudson-Odoi, nafasi au hatma ya Sanchez inaweza kuwa ndogo zaidi kwa siku zijazo.
3- Fred anbaye alisainiwa kwa pound milioni 52 na Matteo Darmian hawa kuna dalili nyingi kuwa hawatakuwa na nafasi kubwa ya kucheza chini ya Ole Gunnar Solskjaer, hivyo kama kapewa mkataba wa miaka mitatu inadaiwa hawezi kuendelea kuweka rehani nafasi zao, Matteo Darmian anatajwa kuwa na mpango wa kurudi Italia.
4-Marcos Rojo kwa mujibu wa sera za usajili wa wachezaji wa kigeni wa Man United, huyu aliongezewa mkataba mwaka uliopita lakini amekumbana na wakati mgumu kiasi cha kuanza mechi nne tu tena sio chini ya utawala wa Ole Gunnar Solskjaer, hivyo inawezekana akaondoka.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars