Kuchelewa kuanza kwa msimu wa mvua za vuli na masika katika maeneo ya hifadhi ya taifa ya Serengeti na maeneo mengine nchini kumetajwa kuathiri mzunguuko wa kiekolojia wa uhamaji wa Nyumbu na Pundamilia ikiwa ni moja ya matukio ambayo yameipa hifadhi ya Serengeti sifa ya kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili ya dunia.
.
Tukio la uhamaji wa nyumbu na wanyama wengine kutoka upande mmoja wa hifadhi ya Serengeti kuelekea upande mwingine wa hifadhi hiyo na hatimaye hifadhi ya masai mara nchini Kenya kupitia eneo la Kogatende Kaskazini mwa Serengeti kwa kawaida hutegemea sana upatikanaji wa maji na malisho katika maeneo hayo.
.
Mtaalamu wa Kieokolojia Julieth Lyimo ameizungumzia hiyo “Kwa kipindi hiki cha mwezo March nyumbu wameanza kusogea mwezi Februari wanakuwa upande wa Kusini lakini wanaanza kuhama kuelekea upande wa katikati ya hifadhi ambapo itaenda hadi Mwezi April kwenda mwezi May makundi makubwa yanakuwa katikati ya hifadhi”>>>Julieth Lyimo
MAMBO MATATU YA MSTAAFU MKAPA KWA WASOMI WA UDOM