Club ya Man United usiku wa January 29 2019 ilikuwa nyumbani Old Trafford kucheza game yake ya 24 ya Ligi Kuu England msimu wa 2018/19 dhidi ya wageni wao Burnley, Man United ambayo kwa sasa inaaminika morali ya wachezaji hiko juu na wakitarajiwa kupata matokeo chanya kila game wamekutana na matokeo ya kushangaza.
Man United wakiwa nyumbani Old Trafford mbele ya mashabiki wao walitarajiwa wapate ushindi kutokana na kuwa na faida ya mashabiki lakini pia rekodi yao chini ya kocha wa mpito Ole Gunnar Solskjaer kucheza game 8 mfululizo chini yake na kushinda zote, kabla ya leo kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2.
Mbele ya mashabiki wao Man United walilazimika kusubiri hadi dakika ya 92 ndio wakihakikishie walau kuvuna point moja na kujinusuru na aibu ya kupoteza nyumbani, kwani tayari Burnley walikuwa wameshapata magoli mawili ya wali kupitia kwa Barnes dakika ya 51 na Chris Wood dakika ya 81 ila Man United walizanza kupata goli dakika ya 87 kwa penati kupitia Paul Pogba na baadae Lindelof aliyefunga goli la kusawazisha dakika chache kabla ya game kuisha.
Ukimuuliza Ajib wa Yanga ishu ya Beno Kakolanya atakujibu hivi