Mbunge wa Mtama Nape Moses Nnauye Jumamosi ya December 15 2018 amehitimisha fainali za kwanza za michuano ya Nape Nnauye Super Cup iliyokuwa inashirikisha timu mbalimbali kutoka katika jimbo lake la Mtama, ila Jumamosi ya December 15 ndio fainali kachezwa.
Michuano hiyo ambayo imethibitishwa kuwa itakuwa inafanyika kila mwaka, leo ilizikutanisha timu za Nahukahuka ya kutoka tarafa ya Nyangamala na Majengo FC kutoka kijiji cha Mtama ilimalizika kwa Majengo FC kuwa Mabingwa wa kwanza wa kihistoria kwa kuifunga Nahukahuka kwa magoli 3-1.
Licha ya michuano hiyo kufanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Mtama lakini ilipata nafsi ya kuhudhuriwa na watazamaji wengi, kiasi cha kuzidisha mvuto wa mchezo huo, Nape Nnauye ameahidi pia michuano hiyo mwakani itakuwa na maboresho makubwa zaidi lengo kuleta mvuto na hamasa kwa vijana na kukutanishwa kwa pamoja na mchezo huo wa soka.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe