Club ya Ismaily ya Misri leo jioni imetangaza good news kwa soka la Tanzania baada ya kuthibitisha kumpatia mkataba mshambauliaji wa kitanzania Yahaya Zayd kutokea club ya Azam FC ya Tanzania, Zayd aliondoka siku mbili zilizopita na kwenda Misri kusaini mkataba wa timu hiyo.
Zayd amesaini mkataba wa kuichezea Ismaily moja kwa moja pasipo kufanya majaribio, hiyo inatoka na uongozi wa club hiyo kumfuatilia mapema akiwa Azam FC kabla ya kuamua kumpa mkataba wa kuichezea timu yao, hivyo kutokana na umri wa mchezaji huyo kuwa mdogo wanaamini atawafanyia makubwa.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anaungana na wachezaji wengine kutoka Namibia na Nigeria waliosajiliwa hivi karibuni kuboresha kikosi cha Ismaily katika michuano mbalimbali ikiwemo hatua ya Makundi ya CAF Champions League waliyopangwa Kundi C na timu za Costantine ya Algeria, TP Mazembe ya Congo na Club Africain ya Tunisia.
Mbona Jonas Mkude hatumuoni Zenji? Meneja wa Simba kajibu