Kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2019/2020, Jumamosi hii saa moja usiku uwanja wa Taifa Dar es Salaam utachezwa mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC, kuelekea mchezo huo kocha msaidzi wa Azam FC Iddi Cheche ameongea na waandishi wa habari.
“Nashukuru Mungu tuko vizuri na vijana wamejiandaa na tumepata mashindano kidogo ya CECAFA yamejaribu kuwajenga vijana wetu kwa sababu tuna maingizo mapya na vijana tumepandisha na wamepata mazoezi ya kutosha, majeruhi tunao Aggrey Morrsi aliyeumia timu ya taifa na Mudathir lakini wanaendelea vizuri”>>>Iddi Cheche
VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS