Wakati Simba SC ikicheza michezo ya kirafiki kwa ajili ya kujiweka fiti zaidi katika mechi za Ligi Kuu, timu ya Bandari FC ya Mombasa Kenya yenyewe ili utumia mchezo huo kama njia ya maandalizi ya kuelekea mchezo wao wa play off dhidi ya Horoya AC ya Guinea.
Baada ya Bandari FC kupoteza mchezo huo kwa kufungwa 1-0 na Simba SC goli ambalo lilifungwa na Ibrahim Ajib dakika ya 78, kocha wao ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga Ben Mwalala ameongea kuwa mchezo huo ndio ulikuwa wa maandalizi yao na Horoya AC ambayo inachezewa na mchezaji wa zamani wa Yanga SC Heritier Makambo.
“Sioni kama nimepoteza mchezo ilikuwa ni mechi ya kirafiki ya kupimana nguvu na matokeo ya mwisho hayakuwa na maana, ilikuwa ni kuangalia perfomance ya wachezaji kabla ya kuelekea mchezo dhidi ya Horoya kule Guinea”>>> Ben Mwalala
VIDEO:AJIB BWANA MIPANGO !!! KAANZISHA MOVE NA KWENDA KUFUNGA