Nikusogee salamu za nguvu za sikukuu ya mwaka mpaya kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, amewatakia watanzania wote heri ya mwaka mpya 2018, huku akiwataka kuendelea kuchapa kazi.
President JPM kupitia ukurasa wake wa twitter ameweka picha yenye ujumbe huo wa mwaka mpya, na kuwaomba Watanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano,pamoja na kufanya kzi kwa bidii ili kujenga nchi.
Namnukuu JPM “Ndugu zangu Watanzania, nawatakia heri ya mwaka mpya 2018, naungana nanyi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake, nawaomba tuendelee kudumisha amani, upendo, mshikamano wetu na tuchape kazi kwa juhudi na maarifa, kwa maendeleo ya Taifa letu ili tujenge Tanzania mpya, umeandika ujumbe huo.
— Dr John Magufuli (@MagufuliJP) December 31, 2017
JPM AWASILISHA TAARIFA YA MALI ZAKE NA AKAUNTI YA BENKI SEKRETARIETI YA MAADILI, BONYEZA PLAY KUTAZAMA
JPM ALIVYOKUTANA NA KAMATI YA KUKAGUA MALI ZA CCM