Michuano ya Mapinduzi Cup 2019 imeanza leo lakini kwa mwaka huu inashirikisha jumla ya timu 9, hiyo ni baada ya URA ya Uganda na Bandari ya Kenya kunyimwa ruhusa na mashirikisho yao ya soka kuja kushiriki michuano hiyo.
Kwa upande wa Tanzania bara safari hii unawakilishwa na timu tatu pekee tofauti na mwaka jana zilikuwa timu nne, timu ambazo zinaiwakilisha Tanzania bara katika michuano hiyo ni Simba SC, Azam FC ambao ndio Mabingwa watetezi na Yanga SC.
Katibu wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo Hamis Said ameeleza kuwa sababu iliyofanya Tanzania bara timu tatu tu kupewa nafasi ni kutokana na muda kuwa mchache ndio maana timu za KMC ya Kinondoni, Mtibwa Sugar na Singida United licha ya kuomba lakini wameshindwa kuzikubalia.
VIDEO: Furaha ya ushindi Kocha wa Simba kashangilia hadi kavua shati