Mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akiwa USA katika NBA All Stars 2019 amefanikiwa kukutana na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast aliyekuwa anaichezea club ya Chelsea ya England Didier Drogba na kujadili mambo kadhaa kuhusu uwekezaji katika michezo.
Kusaga alithithibitisha kutumia ukurasa wake wa instagram kwa kupost picha akiwa na staa huyo na kueleza waliyozungumza “Nimekutana na @didierdrogba – Didier Drogba. Drogba anaamini uwekezaji kupitia michezo unatakiwa na utasaidia sio kwenye kuwapa vijana nafasi bali pia kukuza uchumi wa mataifa husika. Akiwa tayari kuwa sehemu ya uwekezaji wa waliokuwa tayari, Nimemwambia Tanzania tutakuwa wa kwanza kumwita na ameridhia. #nbaallstars2019“
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Didier Drogba ambaye alikuwa nahodha wa Ivory Coast hadi anastaafu kucheza soka la ushindani alikuwa amecheza jumla ya vilabu nane lakini club ya Chelsea ndio ameichezea kwa mafanikio na muda mrefu zaidi (2004-2012) baadae akarudi tena (2014-2015).
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba