Baada ya uwepo wa hofu kuwa staa wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo anaweza akawa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwa hofu ya kupata majeruhi ya enka Jumapili iliyomalizika, leo zimetoka taarifa njema kwa mashabiki wa Juventus kuhusiana na hali ya staa huyo ambaye ni tegemeo kwa Juventus.
Ronaldo aliumia akiwa Juventus weekend iliyopita wakiifunga Bogna 1-0, wanaendalea kulinda point za0 13 zinazowafanya waongeze Serie A kwa tofauti hiyo ya point, hivyo Ronaldo alilazimika kufanyiwa vipimo vya afya ili kuweza kubaini hali yake siku ya Jumatano na leo taarifa za hali yake zimetoka rasmi kuwa yupo fiti.
Juventus wamethibitisha kuwa staa wao Cristiano Ronaldo amerudi mazoezini kama kawaida, Ronaldo baada ya kuanza mazoezi na kugundulika kuwa hakuwa kaumia sana, anaripotiwa kuwa atakuwa sehemu ya mchezo wa Juventus dhidi ya Napoli weekend hii, Ronaldo toka amewasili Turin akiwa na Juventus amefunga jumla ya magoli 21 na kutoa assist 12 katika mashindano yote.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake