Ikiwa imepita siku moja toka uongozi wa club ya AS Monaco ya Ufaransa utangaze rasmi kumsimamisha kazi aliyekuwa kocha wao mkuu Thierry Hnery, leo imetangaza taarifa mpya kuhusiana na msimao wao kuwa ni wamemfuta kazi rasmi kocha wao Thierry Hnery kufuatia mfululizo wa matokeo mabovu.
Kilichowashangaza wengi ni baada ya kumfuta kazi Henry wamemtangaza kocha wao wa zamani Leandro Jardim kuwa ndio kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka miwili na nusu, AS Monaco walimfuta kazi Jardim miezi mitatu iliyopita na kumpa kazi Henry na leo wamemfuta kazi Henry ikiwa zimepita siku 104 toka wamuajiri na kumrudisha Jardim.
Henry ambaye alikuwa na mkataba na AS Monaco hadi mwaka 2021 alijiunga na AS Monaco mwezi October na kuanza harakati za kuipambania timu hiyo bila mafanikio na hatimae kujikuta akifungwa katika michezo 11 kati ya 20 aliyofundisha timu hiyo na kuambulia sare game 5 na ushindi game 4 ila inaelezwa kuwa wachezaji walishinikiza arudishwe Jardim na hawamtaki Henry.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”