Baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya Rwanda kwa sare ya 0-0, baadhi ya watu walianza kuhoji kuhusiana na kiwango alichokionesha mshambuliaji wa Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa England katika club ya Blackpool ya England ila akiwa kwa mkopo kwa sasa Solhull Adi Yussuf.
Unajua baada ya kucheza game ya mwisho ya makundi ya AFCON dhidi ya Algeria katika uwanja wa Alsalaam nchini Misri, wengi waliona Adi Yussuf ni mshambuliaji mzuri kutokana na alivyocheza ila wakashangaa katika mchezo dhidi ya Rwanda hakuonesha kiwango kizuri sana tofauti na matarajio.
Leo Amplifaya ya Clouds FM imempata Adi Yussuf katika exclusive interview na kumuuliza amepatwa na nini, amesikia comment za baadhi ya watanzania wanaolalamikia kiwango alichokionesha dhidi ya Rwanda.
AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI