Kocha mkuu wa club ya ya Singida United Hemed Morocco amesema licha ya kutokuwa kwenye benchi la ufundi la timu yake kwa wiki kadhaa, yeye bado ni muajiriwa wa Singida United ila kinachomfanya ashindwe kuwa nao kwa sasa ni majukumu ya kitaifa.
Morocco ambaye ni kocha msaidizi wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Emmanuel Amunike, amesema kutokuwepo kwake kwenye benchi la ufundi la Singida United hakumaanishi kazi haziendi, bali amekua akifanya mawasilino ya mara kwa mara na wasaidizi.
Kocha huyo ambaye alikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar Zanzibar Heroes hadi kufika hatua ya fainali katika michuano ya CECAFA Senior Challenge 2017, amesisitiza jukumu lingine la kitaifa alilonalo kwa sasa la kuhakikisha kikosi cha taifa chini ya umri wa miaka 23 (Ngorongoro Heroes) kinafanya vyema kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Burundi.
Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19