Michuano ya Euro 2016 imeendelea tena usiku wa June 14 2016, kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa Stade Geoffroy-Guichard kati ya Ureno dhidi ya timu ya taifa ya Iceland, huo ni mchezo ambao umechezwa baada muda mchache kuchezwa mchezo kati ya Austria dhidi ya Hungary katika uwanja wa Stade Matmut-Atlantique.
Mchezo wa Ureno dhidi ya Iceland ndio ulikuwa mchezo wa mwisho kukamilisha hatua ya makundi raund ya kwanza, katika mchezo huo Ureno walikuwa wanapewa nafasi ya kuondoka na point tatu kutokana na hali yao ya umiliki wa mpira kuwa asilimia 66 kwa 34 dhidi ya Iceland.
Hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, licha ya kuwa Ureno walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 31 kupitia kwa Luis Nani na kuendelea kuutawala mchezo, kujisahau kwao kulifanya Iceland kusawazisha goli dakika ya 51 kupitia kwa Birkir Bjarnason na kuwafanya walinde goli lao zaidi.
VIDEO YA MAGOLI YA URENO VS ICELAND
https://youtu.be/v2Y5Aidu9M4
ALL GOALS: Yanga vs Al Ahly (Full Time 1-1) April 9 2016 CAF
https://youtu.be/VSM0_i0-DY0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE