Takwimu kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Ukame ya Kenya (NDMA) zimeonyesha kuwa idadi wa watu wa Kenya wanaohitaji msaada wa kibinadamu imeongezeka hadi milioni 2.
Wengi wa watu wanaohitaji msaada ni wale waathirika wa mvua za El Nino zilizoanzia mwezi Oktoba hadi Desemba mwaka 2023 katika maeneo 23 yaliyo kame na nusu kame nchini humo.
Hadi mwishoni mwa mwezi Januari, NDMA ilikadiria kuwa idadi ya watu wanaohitaji msaada imefikia milioni 1.5.
NDMA pia imesema utapiamlo mkali umetokea kwenye kaunti mbalimbali, ambapo watoto 847,932 wenye umri wa miezi 6 hadi 59 na wajawazito na wanawake wanaonyonyesha 124,359 wana utapiamlo mkali na kuhitaji matibabu.