Idadi ya waliofariki kutokana na ghasia zinazoendelea nchini Afrika Kusini imepanda na kufikia Watu 212 kutoka vifo 117 vilivyoripotiwa awali.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Khumbudzo Ntshavheni amesema vifo vipya vimetokea katika jimbo la kusini mashariki la KwaZulu-Natal ambalo ndiyo kitovu cha machafuko ya sasa.
Hata hivyo amesema hali ya utulivu imeanza kurejea na hadi sasa zaidi ya Watu 2,500 wamekamatwa kutokana na vurugu za karibu wiki nzima zilizohusisha uporaji wa mali na uchomaji wa moto majengo ya biashara.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema vurugu hizo ambazo zimelitikisa taifa hilo zilipangwa na ameapa kuwasaka wote walihusika———“Ni wazi kwamba matukio yote haya yalichochewa, kulikuwa na Watu waliopanga na kuyaratibu”.