Mashambulizi ya kijeshi ya Israel katika Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya Wapalestina 33,899 na kujeruhi 76,664 tangu Oktoba 7, maafisa wa afya katika eneo la Palestina linalotawaliwa na Hamas wamesema.
Wapalestina 56 wameuawa na 89 kujeruhiwa katika muda wa saa 24 zilizopita, maafisa hao waliongeza katika taarifa yao ya kila siku.
Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Israel viliripoti kuwa sehemu ya kurushia kombora na miundombinu kadhaa ya “kigaidi”, ikiwa ni pamoja na mahandaki na majengo ya kijeshi ya Hamas yalipigwa katika mashambulizi ya anga na mizinga ya Israel katikati mwa Ukanda wa Gaza.
Kitengo cha 162 cha IDF pia kiliwaua wapiganaji wa Hamas katika “uvamizi sahihi” katikati mwa Gaza siku ya Jumanne, gazeti la Jerusalem Post liliripoti, likinukuu Vikosi vya Ulinzi vya Israel.
Israel imekuwa ikianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza kulipiza kisasi dhidi ya uvamizi wa Hamas kupitia mpaka wa kusini wa Israel tarehe 7 Oktoba 2023, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na zaidi ya 200 walichukuliwa mateka.