Wizara ya afya huko Gaza inayoendeshwa na Hamas ilisema Jumatatu kuwa watu wasiopungua 33,797 wameuawa katika eneo la Palestina wakati wa zaidi ya miezi sita ya vita.
Idadi hiyo inajumuisha takriban vifo 68 katika muda wa saa 24 zilizopita, taarifa ya wizara hiyo ilisema, na kuongeza kuwa watu 76,465 wamejeruhiwa katika Ukanda wa Gaza tangu vita vilipoanza wakati wapiganaji wa Hamas waliposhambulia Israel tarehe 7 Oktoba.
Wakati hayo yakijiri hii leo waziri Mkuu wa Israel Binyamin Netanyahu saa mbili usiku (1100 GMT) atakutana tena na bapia raza lake la mawaziri la vita, jukwaa lililopewa mamlaka na mawaziri wengine kuamua juu ya hatua zozote za kukabiliana na shambulio la wikendi la Iran, chanzo cha serikali kilisema.
Baraza la mawaziri la vita, linalojumuisha Netanyahu, Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant, waziri wa zamani wa ulinzi Benny Gantz na waangalizi kadhaa, awali walikutana Jumapili usiku.