Idadi ya watoto waliofariki katika tukio la kukanyagana wakati wa tamasha la watoto huko Ibadan, mji mkuu wa mkoa wa Oyo, kusini magharibi mwa Nigeria imeongezeka na kufikia 35.
Msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Adewale Osifeso amewaambia wanahabari mjini Ibadan kwamba, mpaka sasa watoto 35 wamethibitishwa kufa, huku wengine 6 wakiwa na majeraha mabaya na wanaendelea kupata matibabu.
Amesema kesi hiyo imehamishiwa katika kitengo cha upelelezi wa mauaji katika Idara ya Upelelezi wa Uhalifu ya Iyaganku, na inaongozwa na Naibu Kamishna wa Polisi, na kuongeza kuwa, mpaka sasa watu wanane waliotambuliwa kuwa waandaaji wa tamasha hilo wanashikiliwa na polisi.