Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Frelimo manispaa ya Iringa Dkt . Hassan Mtani amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha fedha cha zaidi ya milioni 247 kwaajili ya ujenzi wa wodi ya watoto na kukamilisha miundombinu ya kuongeza bajeti ya vifaa tiba ili kuweza kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto
Hayo yamesemwa leo na Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Frelimo Dkt Hassan Mtani wakati akitoa taarifa kwa mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu CCM Taifa Mhe Abood Mohamed Abood ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa alipotembelea hospitalini hapo.
Kwa mwaka 2022 akina mama 700 waliojifungua katika hospitali yetu kati yao kulitokea na kifo kimoja tu ambacho kilitokana na kifafa cha mimba na vifo vimepungua ukilinganisha na kipindi cha nyuma
Akizungumza na watumishi wa Hospitali hiyo mjumbe wa kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa mhe. Abood Mohamedi Abood amewahimiza watumishi wa Afya kuzingatia weledi wakati wa kazi na maadili katika utoaji wa huduma za afya.