Labda hii Ripoti itasaidia kujifikiria mara mbilimbili kwa wale Dada zetu ambao walikua wanampango wa kwenda kufanyiwa upasuaji utakaopendezesha miili yao iwe ni sura, tumbo, hips au makalio.
Ripoti mpya ya Jarida la The Gurdian imeonesha kwamba takriban Wanawake 100 hufariki kila mwaka duniani wakati wakifanyiwa upasuaji wa kupendezesha miili yao.
Wengi hufanya upasuaji wa kuongeza au kurekebisha maziwa, wengine kurekebisha tumbo, wengine uso lakini Wataalamu wanasema upasuaji ambao ni hatari zaidi ni ule wa kuongeza hips na makalio.
Pamoja na kwamba mara nyingi kifo ni kimoja katika Wanawake 300 wanaofanyiwa upasuaji wa hips na makalio, wanaothirika idadi yao ni kubwa ambapo kwenye hao 300 kuna wengi ambao hata kama hawajafa ila hawatopata matokeo waliyoyategemea na wengine hupata kansa kadri umri wao unavyoongezeka.