Tangu vita kuanza kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha wanamgambo cha RSF mwezi Aprili 2023, watu wapatao 300,000 wamekuwa wakiishi katika kambi ya Zamzam jirani na mji mkuu wa mkoa wa Darfur ya Kaskazini ambao haujakuwa ukipokea misaada ya kibinaadamu wala kuwa na uwezo wa kutoa huduma za afya.
Katika taarifa ya Jumatatu, MSF imesema inakadiria kuwa kuna vifo vya watoto takriban 13 kila siku, kulingana na tathimini ya dharura kuhusiana na lishe na vifo iliyofanywa Januari.
Waatalamu wanasema utapia mlo wao unatibika endapo, wataweza kufika katika vituo vya afya, lakini kutokana na upungufu wa msaada wa dharura, hali inazidi kuwa mbaya na kusababisha ongezeko la vifo.
Katika utafiti wa familia 400, MSF imegundua kiwango cha vifo 2.5 kwa kila watu 10,000 kwa siku katika kambi, mara mbili ya kiwango kilichozaniwa kuhitaji msaada wa haraka.