Wizara ya afya huko Gaza ilisema Jumanne kwamba watu 21 wameuawa katika eneo la Palestina katika masaa 24 yaliyopita, na kufanya jumla ya vifo vya vita kufikia 45,338.
Wizara hiyo pia ilisema katika taarifa yake kwamba watu wasiopungua 107,764 wamejeruhiwa katika zaidi ya miezi 14 ya vita kati ya Israel na Hamas, vilivyochochewa na shambulio la kundi la Palestina la Oktoba 7, 2023.
Usitishaji vita kati ya Israel na Hamas bado unaonekana kuwa mbali. Vyombo vya habari nchini Israel vimeripoti kuwa mazungumzo juu ya makubaliano ya kusitisha vita na kuachiliwa kwa mateka katika Ukanda wa Gaza yamepiga hatua fulani, lakini hoja zinazosababisha kutofautiana zingalipo, kama vile ni mateka wangapi Hamas itawaachilia.