Idadi ya watu ambao wamepoteza maisha kutokana na mafuriko nchini Kenya imeongezeka hadi 188, wizara ya mambo ya ndani ilisema Alhamisi, huku nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na mvua kubwa.
Maeneo mengi ya taifa hilo la Afrika Mashariki yameharibiwa na mvua, mafuriko na maporomoko ya ardhi ambayo yameharibu barabara, madaraja na miundombinu mingine.
“Matokeo yake, nchi imeandika kwa masikitiko vifo 188 kutokana na hali mbaya ya hewa,” wizara ilisema katika taarifa.
Imeongeza kuwa watu 125 wameripotiwa kujeruhiwa na watu 90 hawajulikani walipo, huku 165,000 wakiwa wamelazimika kuyahama makazi yao.