Idadi ya watu waliofariki katika mlipuko wa lori la mafuta uliotokea katikati ya Liberia imeongezeka na kufikia watu 40.
Afisa Mkuu wa Afya nchini humo Francis Kateh, amesema watu wengine wengi wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo uliotokea baada ya lori la mafuta kupinduka na kuanguka kwenye mtaro kando ya barabara mjini Totota, Kaunti ya Bong.
Amesema huenda idadi ya watu waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea Jumanne ikaongezeka kutokana na hali mbaya ya majeruhiwa waliolazwa hospitalini.