Wizara ya afya inayoongozwa na Hamas inasema idadi ya watu waliouawa Gaza tangu kuanza kwa vita imeongezeka hadi 10,569.
Hilo ni ongezeko la 241 kati ya vifo 10,328 vilivyoripotiwa jana.
Kati ya hao, 4,324 ni watoto, wizara ilisema, na wengine 26,457 wamejeruhiwa.
Takwimu za hivi punde zaidi za UNRWA zinaonyesha zaidi ya watu 700,000 wamekimbia makazi yao huko Gaza tangu tarehe 7 Oktoba, wakati wapiganaji wa Hamas walipofanya mashambulizi makubwa ndani ya Israel, na kusababisha mashambulizi makali ya kulipiza kisasi.
Israel imesisitiza kuwa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha raia wanawekwa salama huko Gaza – kwa kufungua korido za kibinadamu, kuacha vipeperushi na kupiga simu kuwataka watu, haswa kaskazini, kuhama.