Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, idadi ya waliouawa kwa mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya eneo hilo imefikia 41,000.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la IRIB, Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, idadi ya wahanga wa mashambulizi ya adui mzayuni Israel kwenye Ukanda wa Gaza imeongezeka na 40,972 waliouawa shahidi na 94,761 elfu waliojeruhiwa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, “katika saa 24 zilizopita, wavamizi wa Kizayuni wamefanya mauaji matatu mapya dhidi ya familia katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha kuuawa shahidi watu 33 na kujeruhiwa 145.