Idadi ya watu waliouawa Gaza na mashambulizi ya anga ya Israel imeongezeka hadi 9,061, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas.
Miongoni mwa waliofariki ni watoto 3,760 na wanawake 2,326, msemaji wake alisema.
Watu wengine 32,000 walijeruhiwa, alisema msemaji huyo.
Hii inamaanisha kuwa idadi ya vifo imepanda kwa zaidi ya watu 260 tangu sasisho la mwisho la wizara ya afya, hapo jana, iliposema watu 8,796 wamekufa – 3,648 kati yao watoto.