Jamii imetakiwa kuhakikisha inachukua hatua katika kukabiliana na kasi ya ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi Mkoa wa Mwanza, ambapo takwimu zinaonesha kutoka asilimia 4.2 hadi kufikia 7.2, hasa kundi la vijana na rika balehe ambalo taifa linawategemea.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Amina Makilagi ambae ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana wakati wa kupokea vifaa vya teknolojia ya uhifadhi takwimu na kumbukumbu kwa njia skana njia ya vidole kutoka shirika la ICAP la nchi Marekani amesema vifaa hivyo vitasaidia kuweka usiri wa taarifa za Mgonjwa tofauti na mwanzo taarifa zilipitia kwa watu zaidi ya watu wa tatu.
Dkt. John kahemele ni Naibu Mkurugenzi mkazi shirika la ICAP Tanzania, anaeleza kutokana na ongezeko la watu wanaoishi na maambuziki ya virusi vya Ukimwi kwa mkoa wa Mwanza, shirika hilo imefanya juhudi za kufikisha tiba na matunzo kwa watu wenye maambukizi.