Idadi ya watu nchini Niger imeongezeka kwa 20% katika robo ya kwanza ya mwaka huu, ikilinganishwa na miezi mitatu iliyopita ya mwaka 2022, inabainisha ripoti hii ya IOM huku theluthi moja ya idadi hii wanabaki nchini Niger, wale wanaosalia huvuka mpaka, iwe ni kuingia au kutoka nchini humo.
Data inakusanywa kutoka kwa wasafiri katika sehemu kumi za kuvukia ili kuchanganua mienendo ya uhamaji huu.
Ongezeko hili, kwa mujibu wa ripoti hii, linaelezewa na watu waliohamishwa kuelekea maeneo ya dhahabu na kufukuzwa kwa wahamiaji kutoka Algeria na Libya.
Idadi kubwa ya watu walioangaliwa na timu za IOM kati ya mwezi Januari na mwezi Machi ni wanaume watu wazima. 18% ni wanawake, 9% ni watoto wadogo ambao wanatoka hasa nchini Niger au nchi jirani, na hasa wakitoa sababu za kiuchumi za kuhama kwao.
Mamia ya watu walikufa au kutoweka kwenye njia zisizo halali wanazotumia wahamiaji kwa kuvuka kutoka Niger hadi Afrika Kaskazini, kupitia jangwani, katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu.
Hili ndilo linalojitokeza kutokana na ripoti ya wimbi la idadi ya watu nchini Niger, iliyochapishwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), kupitia Mfumo wake wa Kufuatilia watu wanaohama kutoka eneo moja kwenda lingine.