Idadi ya watu waliouawa katika mashambulio dhidi ya vijiji katikati ya Nigeria imeongezeka na kufikia 200.
Mamlaka za eneo hilo zimesema, makundi yenye silaha yalifanya mashambulio hayo kati ya jumamosi jioni na jumanne asubuhi katika mkoa wa Plateau nchini Nigeria.
Akizungumza na makamu wa rais wa Nigeria jana jumatano mjini Bokkos, mkuu wa serikali ya mkoa wa Plateau Monday Kassah amesema wanakijiji 148 wa Bokkos wameuawa katika mashambulio hayo.
Wakati huohuo, mwakilishi wa mkoa huo Dickson Chollom amesema, watu wengine 50 wameripotiwa kuuawa katika vijiji kadhaa vilivyoko eneo la Barkin Ladi.