Jeshi la Israel (IDF) limesema limemuua naibu mkuu wa propaganda wa Palestina Islamic Jihad katika shambulio la anga siku ya Alhamisi.
Ilisema Wael Abu Fanounah alikuwa na jukumu la kutoa video za propaganda za mateka na kunakili picha za milio ya roketi dhidi ya Israel.
Katika taarifa ya pamoja, IDF na Shin Bet hawakusema operesheni hiyo ilifanyika wapi.
Walimshutumu Abu Fanounah kwa kuwa aliwahi kuwa naibu wa Khalil Bahtini, naibu kamanda wa Palestina Islamic Jihad kaskazini mwa Gaza.