Mbali na mzozo wa Gaza, Jeshi la Ulinzi la Israeli linasema kuwa limeshambulia safu ya shabaha za kundi la Lebanon la Hezbollah, kundi la Kiislamu la Shia linaloungwa mkono na Iran ambalo lina nguvu kubwa ya kijeshi na kisiasa nchini Lebanon.
Inachukuliwa kuwa shirika la kigaidi na Israel, Uingereza, Marekani na wengine.
IDF inasema jeshi lake la anga lilishambulia miundombinu kadhaa ya kigaidi pamoja na maeneo ya kijeshi ambapo magaidi wa shirika hilo waliendesha shughuli zao.
Tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi yake dhidi ya Gaza kufuatia shambulio la Hamas tarehe 7 Oktoba, Hezbollah mara kwa mara imekuwa ikifanya mashambulizi ya roketi na ndege zisizo na rubani kutoka kusini mwa Lebanon, baadhi yakilenga maeneo ya kijeshi, mengine yakirusha kiholela kaskazini mwa Israel.
Israel imewahamisha maelfu ya raia kutoka eneo hilo kwa sababu ya kuongezeka uhasama na wanamgambo wa Hezbollah.