Kampuni ya ScotRail Alliance huko Scotland imetoa ofa ya kuwasafirisha bure watu wote ambao wanatafuta ajira pale wanapokwenda kufanyiwa usaili kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni kuwapeleka na kuwarudisha.
Ofa hii pia ni kwa wote waliopata kazi tayari kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kupata kazi, lengo ikiwa ni kupunguza gharama za usafiri kwa ambao hawana ajira huku wakiwasaidia kufanikiwa kwenye usahili wa kazi.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Alex Hynes ameeleza kuwa msaada huo utasadia kuboresha uchumi wa Scotland kwani gharama ya kusafiri inaweza kuwa kuzuizi kwa watu wanaojaribu kutafuta ajira.
Umepitwa na hii? Agizo la Waziri Mwigulu “Tusitafute ugomvi na Serikali za Nchi hizi…”