Raia tisa wa Tanzania pamoja na raia wawili wa Msumbiji wameuawa na watu wasiojulikana huku Watanzania wengine sita wakijeruhiwa katika kijiji cha Mtole kilichopo upande wa Msumbiji mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchni, IGP Sirro amefika mkoani Mtwara kufuatilia tukio hilo lililotokea June 26, 2019.
“Nasikitika kwa vifo vya Watanzania, hatutokuwa na muhali na Muuaji akipatikana hata akitangulia mbele za haki kwangu ni sawa, nitajibu mbele za haki, uwezo tunao tutatumia Interpol na sheria zilizopo kuhakikisha waliofanya mauaji wanapatikana wakiwa salama au wamefariki”-IGP Sirro
“Na bahati mbaya taarifa tulizopata wanaofanya haya mauaji wanazungumza Kiswahili kizuri sana, wengi ni wale waliokimbia huku kwetu baada ya kupata moto mkali, hawa watu wa hovyohovyo wanauliza wewe Mtanzania ukijibu ndio wanawapiga risasi” – IGP Sirro
“Timu zetu za oparesheni zinapita maeneo mbalimbali kuhakikisha maeneo yetu, Mtwara yetu inakuwa shwari, Kijiji ambacho wameletwa kule ambako wamezikwa nimetoa maelekezo tutakuwa na doria ya kutosha maeneo yale mpaka hali itakapokuwa shwari” – IGP Sirro