Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa si kweli kwamba Askari wa Usalama Barabarani, wanatoza faini za makosa ya usalama barabarani ili waweze kutimiza malengo waliyowekewa ya kukusanya mapato kila siku na kukuza pato la Taifa.
“Kuna hili suala lilikuwa linazungumzwa kwamba inawezekana tumeweka ‘target’ kwamba lazima kila mtu akusanye kiasi fulani cha pesa, Watanzania wenzangu hiyo biashara haipo, ni kwamba faini zinazotozwa ni kutokana na makosa yaliyotendwa barabarani wala hakuna target kwamba kila siku lazima Askari apate kiasi fulani ili kuongeza pato la Taifa”, IGP Sirro.
“Kule Mtwara tunakwenda vizuriu, timu zetu zipo, niwashukuru sana wananchi wa Mtwara na Lindi wanatupa taarifa za kutosha, na wale huku ndani wanaofanya chochoko tunawakamata wazazi na walezi wajitahidi sana watoto wao wasijiingize kwenye ugaidi, ukishaingia huko ni vita”. IGP Sirro